Kwenye zile stori za Hekaheka leo Geah Habib aliitwa na wanaanchi wa Kivule wakidai kuna jirani yao amekuwa akiwanyanyasa na kutaka kuwachinja.
Watu wengi wamekuwa wakilalamika, kwanza wamesema kuna kiwanja chake ambacho sasa kimekuwa msitu na kuna nyoka wengi ambao wanahatarisha maisha yao lakini kila wakimuomba afyeke huwa anakataa.
Pia kuna siku mke wake alipandisha mashetani na kumtaja mmoja wa majirani zake kuwa anamloga..wakamfuata nyumbani kwake akiwa na familia yake na mapanga wakitaka kumuua wakidai anawaloga.
Familia hiyo iliyovamiwa iliwabidi wakimbilie kituo cha polisi Kivule lakini wanachoshangaa mtuhumiwa na familia yake hawajakamatwa kwa madai Serikali haiamini uchawi..lakini madai yao ni kuvunjiwa nyumba na vitu vyao kuharibiwa sana.
Majirani wamezungumzia manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa mzee huyo na kusema amekuwa akiwanyanyasa sana ikiwemo kuwatishia kuwachinja akishirikiana na watoto wake.
Wanasema imefikia hatua akikuta uchafu katika viwanja vyake pamoja na pori lake anawaambia majirani zake waende kuokota na endapo watatakadi ataenda kuokota mwenyewe na kupeleka ndani ya nyumba zao.
Wamesema wanaiomba Serikali iingilie kati kwani imefikia hatua hata hataki nguzo za umeme zipite karibu na viwanja vyake na huwatoza fedha kubwa ambayo wananchi hawawezi kumudu.
Watoto wake pia wamekuwa wakitumia mapanga na kuwatishia watu kuwauua, pia wamekuwa wakiwatukana kisha kukimbilia kuwashtaki kwa baba yao endapo watawadhuru…kuna jirani mpaka sasa yupo ndani baada ya kugombana na familia yake.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE