Miezi ya hivi karibuni Headlines za ugonjwa wa Ebola zilisambaa katika vyombo mbalimbali vya habari duniani.
Leo headlines zimerudi tena huko Nigeria baada ya watu 10 kuwekwa karantini katika hospitali ya Calabar huku mtu mmoja akifariki baada ya kuwa na dalili zote za ugonjwa huo.
Vyombo vya habari vya Nigeria vimesema mtu huyo alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali.
Hivi karibuni Shirika la afya duniani WHO lilitoa taarifa kuwa nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na Liberia mpaka sasa zimefanikiwa kukaa bila kuwa na tukio lolote la ugonjwa wa Ebola.
Ugonjwa huo ulianza kushika kasi Machi mwaka 2014 na zaidi ya watu 10,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER,FB, YOUTUBE