Kama umewahi kukutana na taarifa mitandaoni, kwenye vyombo vya habari au kwingineko basi ninayo majibu yote kutoka Wizara ya Fedha kuhusu ishu ya ukata wa Fedha Serikalini Tanzania.
Hii ni nukuu ya Kamishna Bajeti wa Wizara ya Fedha akitoa majibu ya pesa zilikotumika >>> “Watu waliokuwa wanaandikisha kupiga Kura, gharama zake ndizo tulizopeleka Tume ya Uchaguzi… Kwa mara ya kwanza katika chaguzi zote zilizowahi kufanyika mwaka huu Uchaguzi umefanywa na fedha za Watanzania.”
Kuna ukweli kuhusu Serikali iliyotoka madarakani kumaliza pesa zote? Majibu haya hapa >>> “Upatikanaji wa fedha uko hivi; hela zinazokusanywa leo zinaingizwa kwenye mfuko mkuu wa Serikali Benki Kuu. Haiwezekani mtu akakomba hela kwa sababu zile hela zinaingia kila siku na kutoka, haiwezekani mtu akombe hela mfuko Mkuu wa Serikali… Kama kuna mtu amekomba hela msingesikia kwamba watumishi wa Serikali wameshindwa kulipwa mshahara? Mngesikia maandamano… tungeweza kufanya uchaguzi wetu wenyewe? vyuo vikuu wangepata hela za mikopo?… JK hakukomba hela hazina.” >>> Kamishna John Cheyo.
Hii hapa sauti niliyoipata kwenye habari ya kituo cha TBC 1 leo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.