Rais wa awamu ya tano Dk.John Magufuli ameendelea na mikakati yake ya kuhakikisha anaiweka nchi katika nafasi nzuri ya kufikia mafanikio ya kimaendeleo.
Ikiwa ni mwezi mmoja tangu achaguliwe kuiongoza nchi katika awamu ya tano, Rais Magufuli ameendelea kukaa kwenye headlines kufuatia maamuzi yake ya kuwaondoa watu wanaotumia vibaya madaraka yao ambayo yanaipeleka nchi katika wimbi la umaskini.
Kaimu katibu mkuu ofisi ya Rais Hab Mkwizu leo amekutana na waandishi wa habari, Dar es saalam na kuzungumzia utekelezaji wa utaratibu wa ahadi ya uadilifu kwa watumishi wote wa umma.
Katika mikakati waliyojiwekea Mkwiu amewakumbusha watumishi wa umma majukumu yao..“Kila mwajiri wa utumishi wa umma anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya Utaalam, uadilifu pamoja na uaminifu, pia anapaswa kuzingatia uzalendo na kuwahudumia wananchi kwa staa, kutoa huduma bora, usawa, kuheshimu sheria na kutumia vizuri rasilimali za Serikali kwa manufaa ya umma”...Hab Mkwizu.
Mwajiri atatekelezaje taratibu za ahadi ya uhadilifu?..”Kila mwajiri katika utumishi wa umma anapaswa kusoma na kuzingatia maelekezo yaliyomo katika waraka wa mkuu wa Utumishi kuhusu ahadi za uadilifu, pia atasaini kiapo kinachohusu watumishi wa umma kwa utaratibu uliowekwa na taasis husika”..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE