Ile kauli ya Rais kuhakikisha anapunguza matumizi yasiyo yalazima kwa Serikali imeendelea kuchukua headlines, pia tumeshuhudia baadhi ya viongozi wakisimamishwa kazi kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma
Leo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amewageukia wakandarasi wa barabara za Manispaa yake ambao imeonekana wametumia kiasi cha fedha za umma kinyume na makubaliano.
Barabara nyingi zimejengwa chini ya kiwango...”Vita kubwa tuliyonayo ni ya matumizi mabaya ya pesa za umma, mwaka huu niliunda kamati ya kuchunguza barabara, matokeo yake wakatupa picha kuwa barabara zetu zimejengwa chini ya kiwango, nimekuja kwenu leo nikiwa na mambo makubwa matatu, ujenzi wa miradi ya barabara kuna pesa mbayo huongezeka kutokana na sababu kadhaa ambayo inatakiwa isizidi 15% ya pesa iliyopitishwa katika mkataba wa awali”..Paul Makonda.
Makandarasi kutolipwa kuanzia sasa…“Nimezuia kuanzia sasa hakuna wakandarasi watakaolipwa katika hizi barabara sita, na nimeagiza siku tano nipate taarifa na nimeelekeza kuandika barua kwa Mkurugenzi, na mafaili yaletwe ofisini kwake, wale watakaobanika watachukulia hatua kali za kisheria”….
Fedha zimetolewa kinyume na utaratibu..“Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kujenga barabara sita za Manispaa ya Kinondoni ni bilioni 4.9 ndio pesa iliyopitishwa, lakini fedha iliyoongozeka ni bilioni 5.7 ambayo haipo kwenye mkataba, zaidi ya bilioni 10 zinahitajika kwa mradi uliopaswa kujengwa kwa bilioni 4..Bodi ya wazabuni walitembelea miradi baada ya kuona wanaomba pesa, walikuta miradi haipaswi kuongezewa pesa, walioomba pesa wakiwa hawana kibali lakini tayari wamelipwa pesa, naitaka hiyo pesa irudishwe haraka iwezekanavyo” Paul Makonda.
“Ziko taratibu za malipo, zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara zetu kwa utaratibu unaotakiwa, kwa hali hii nitaendelea kupigana vita daima na sitakatishwa tamaa na kila anayejiunga na mafisadi, kwa mamlaka niliyonayo ninasitisha ulipwaji wa wakandarasi katika barabara za Mkwajuni-Lion-Biafra-Mabatini-Feza road-Mandaz Road..nataka hatua zichukuliwe, wachunguzi wa mahesabu watoe ufafanuzi kwa hizi fedha zilizozidi”…Paul Makonda.
“Unakuta Barabara ya kujengwa kwa milioni 500 inajengwa kwa bilioni1.3 hii sio sawa, tunahitaji fedha katika mambo mbalimbali kama hospitali, shule na kwingine na si kuwatajirisha watu wachache ambao wanaihujumu nchi yetu”. Paul Makonda.
Sauti ya Paul Makonda akizungumza na waandishi wa Habari..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.