Hoverboard ni jina la kiingereza lakini sina uhakika kama kuna jina rasmi la kiswahili limepatikana kuviita hivi vifaa… ni kama fashion sasahivi utaona mastaa kibao wanapost video wanatembea navyo !! Lakini kama haujaviweza tafadhali mtu wangu, hata usithubutu kuvijaribu..
Ripoti ya stori kwenye mtandao wa BBC inasema waumini kadhaa wamemshutumu Paroko mmoja wa Ufilipino ambae ameonekana akiwa anahubiri kanisani huku akikatisha juu ya hoverboard.
Hii hapa video ya Paroko huyo akikatisha na hoverboard wakati wa ibada ya Christmas Ufilipino ambapo hata uongozi wa kanisa hilo hawakupendezwa na kitendo hicho pia wanachokiona kama kuikosea heshima nyumba ya ibada.
https://www.youtube.com/watch?v=29e1gzNwPFc
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE