Wakati zoezi la Bomoabomoa likiendelea katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam tayari Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetoa mikakati ya kuendeleza bonde la mto Msimbazi.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Bonaventure Baya amezungumzia mipango yao kuwa wana mpango wa muda mfupi kati ya Januari 2016 hadi Juni 2016.
Baada ya Ubomoaji Serikali inategemea kufanya usafi eneo lote kisha kuweka mipaka katika kingo ili liweze kufahamika na kutovamiwa tena.
‘Serikali Itaandaa mpango wa muda mfupi wa matumizi ya bonde la Msimbazi, na tayari Waziri wa ardhi alikwisha agiza wataalamu wakae na kubuni nini kitafanyika baada ya kusafisha eneo lote’...Baya
Pia baada ya Juni Mpango wa muda mrefu utakuwepo ambao ni kufanya bonde liwe la burudani kwa wakazi wa Dar es salaam ambapo utatekelezwa na Wizara ya ardhi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE