Hii stori imekuwa kubwa sana mitandaoni, picha zimesambaa zikionesha mwanamke mmoja aliyekutwa ndani ya shimo maeneo ya Kimara Dar.
Timu ya Leo Tena imefika kwenye tukio na imesimuliwa kila kitu jinsi ambavyo tukio zima limetokea… japo watu wengi wamehusisha tukio hilo na masuala ya ushirikina na mwenye nyumba pia kahusishwa lakini Polisi wamesema sio kweli kwa sababu mwenye nyumba huyo ndio alikuwa wa kwanza kumkuta mwanamke huyo na kutoa taarifa Kituo cha Polisi.
Kamanda wa Polisi Kinondoni amesema walipata taarifa hiyo, wakafika na kutaka kuanza taratibu za kisheria kufungua kesi yake lakini ghafla akatoweka kwenye mazingira ya kutatanisha.
Stori za Hekaheka yote mwanzo mwisho kwenye sauti ya ‘Leo Tena‘ hii hapa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE