Mkali ya fleva za dancehall toka Bongo TZ, Chibwa Man amesema watu wake wanahitaji kumsogeza kwenye level za kimataifa, so kwa sasa mpango unaofatia unaweza kuwa ni kubadili lugha ili atoboe mbali zaidi na muziki wake usikilizwe kwenye level nyingine duniani.
Baada ya kushuhudia wasanii wakitambulika kwenye headlines za kimataifa ni zamu ya producers pia kutoboa, Nahreel anaanza na Patoranking wa Nigeria.
Nahreel amesema alikutana na Patoranking alipokuja TZ kwenye show, akamsikilizisha kazi kadhaa hivi na jamaa akaonekana kupenda mzigo, kamtumia beats kadhaa na huenda ujio wa album ya Pato ukawa na mkono pia wa kazi ya Nahreel… all the best kwa mtu wetu !!
Alikiba amesema kabla ya muziki alikuwa mkali sana kwenye soka, baada ya kuachia ngoma ya Cinderella akaona hata isiwe kesi, shida ilikuwa ni kusaka pesa na pesa zimeanza kuonekana zaidi kwenye muziki akona aachane na soka… ikawa show baada ya shows kuanzia hapo.
Stori na wakali wote ziko kwenye hiio sauti mtu wangu, ni Alikiba, Nahreel na Chibwa Man mwenyewe kwenye 255.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.