Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya habari February 28 2016 millardayo.com inakupatia fursa ya kuzitazama habari kubwa za siku kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka kituo cha Channel 10 Uvuvi Haramu Ziwa Victoria
Katika kukabiliana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi imeteketeza nyavu zilizopigwa marufuku na serikali zenye thamani ya shiling milioni 200.
‘kwa mwaka uliopita serikali ilijipatia wastani wa shilingi bilion 3.6 kila mwaka kwa ajili ya mraba wa mauzo ya mazao ya uvuvi nje ya nchi‘>>>Lameck Mongo Afisa mfawidhi msimamizi wa rasilimali za uvuvi kanda ya ziwa
‘Nilikuwa na mapendekezo kama mtu akikamatwa anatumia nyavu haramu basi achukuliwe kama ni muhujumu uchumi, sheria ileile inayotumika kwa ajili ya wahujumu uchumi itumika kwa ajili ya wavuvi haramu‘ Juma Makongoro Mkuu wa kitengo cha doria kanda ya ziwa
Hari kutoka Clouds TV… Walimu Kusafiri Bure
Walimu wa shule za Serikali kuanzia ngazi ya Msingi hadi sekondari jijini Dar es salaam wanatarajiwa kusafiri bure kwenye usafiri wa umma kuanzia tarehe 7 mwezi wa 3.
‘Ningependa kuwatangazia Walimu na Watanzania kuanzia tarehe 7 ya mwenzi 3 Walimu wa shule za msingi na sekondari watasafiri bure kwenye Mkoa wetu wa Dar es salaam‘>>> Paul Makonda Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
‘Niseme tu tutawabeba walimu kwa utaratibu huo wa vitambulisho lakini pia uwepo utaratibu sasa isionekane basi moja wanaingia watu wa 4 au 5′>>>Makondakta na Madereva
Habari kutoka Clouds TV…Jitokeze kuchangia Damu
‘hili jambo sio la leo tu sisi kama shirikisho tumefanya tunaomba liendelee hata sehemu nyingine tukifanya kama wanafunzi tukijitokeza au jamii ikijitokeza tuna uhakika tatizo la damu litaondoka Tanzania‘>>>Hamiss Mahamud Mchangia damu
‘Tulikuwa tunapata damu 2 hadi 5 lakini sasa hivi tunapata damu mpaka uniti 15 hadi 20 kwa siku kwa hiyo kunaonekana kuna mwamko‘>>>Daktari
Habari kutoka TBC1… Wazee na Viongozi Watakiwa Kumaliza Tofauti Zao
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema Serikali haiko tayari kurudia uchaguzi na badala yake wahusika kukaa na kumaliza tofauti zao’Tuna halmashauri lakini hazijatimia baraza la madiwani haliwezi kukaa, kazi haziendi ndani ya halmashauri ni tatizo kubwa ambalo bado kuna kazi kubwa ya kufanya dhidi ya wana Tanga‘>>>Samia Suluhu Makamu wa Rais
‘Lakini hasara nyingine kwa Tanga mjini ni kuvunjwa kwa halmashauri nzima wasipokaa kitako wazee na viongozi wa Tanga mjini wakamaliza matatizo yaliyopo kuna hatari kwa sababu hatutaweza kurudia uchaguzi‘>>>Samia Suluhu Makamu wa Rais
Habari kutoka ITV… Wanafunzi Wayakimbia Madarasa Kwa Hofu ya Kuangukiwa
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Maisaka katika halmashauri ya mji wa Babati wamelazimika kuyahama Madarasa 4 ya shule kwa hofu ya kuangukiwa na majengo ya shule hiyo.
‘Haya Madarasa ni hatarishi kiasi kwamba yanatokosesha amani hapa shuleni siku yatakayo anguka hatujui lakini siku yakianguka mchana itakuwa ni madhara sana kwa watoto‘>>>Mwalimu
‘Kata hii ina matatizo mengi sana ndio maana tumepita kwenda kuangalia, kwa mfano swala la madawati na viti tumeanza kulishughulikia kwa kuongea na Veta ili warekebishe yale madawati yote ambayo yameharibika‘Paulina Gekul Mbunge wa Babati Mjini
Ulikosa kuangalia Video ya magoli ya Yanga Vs Cercle de Joachim, Full Time 2-0 27/02/2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE