Kwenye game ya bongofleva moja ya stori zilizopita sana juzi kati ni wimbo wa ‘shika adabu yako‘ wa Nay wa Mitego kuripotiwa na vyombo vya habari kwamba umepigwa marufuku kuchezwa kwenye Media kufungiwa na baraza la sanaa Tanzania (BASATA) ambapo taarifa hizo zimemfikia na msanii wa bongofleva Mzungu Kichaa.
Mzungu Kichaa ametoa maoni yake kwa kusema ‘sikutegemea kwamba wimbo wa Nay wa Mitego ungefungiwa, ameongea vitu vya maana… anaongea kuhusu msumeno usiong’ata, pale anawalenga BASATA moja kwa moja lakini ni kitu ambacho inabidi BASATA wawe tayari kukichukua, wasione ni kitu kibaya… hiyo iwe mwanzo wa mazungumzo kujadili kitu, wasifungie tu wimbo‘
‘Napinga kuleta Upolisi kwenye sanaa kama hivi…. mi nimeupenda sana wimbo wa ‘shika adabu yako’ na nilikwenda kusoma mashairi kwanza kabla hata ya kuusikiliza wimbo, sio kwamba nakubali kila alichoandika pale ila ni vizuri kuwa na msimamo na kuongea kitu kinachotokea kwenye jamii ili tukijadili hata kama amesema kitu kibaya’ – Mzungu Kichaa
Ukihitaji kuona yote aliyoyazungumza Mzungu Kichaa bonyeza play kwenye hii video hapa chini…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE