Wataalamu wa mambo wanasema kuna idadi kubwa ya watu wanao uwezo wa kifedha lakini nyumba zao zimekosa mvuto sababu hawakupata mwongozo mzuri wakati wa ujenzi au mipango ya mwanzo ya upangaji wa nyumba.
Unaweza kujaza vitu vingi vya thamani kwenye nyumba na bado isiwe na mvuto ndio maana wataalamu wanashauri upate mwanga wa nyumba za kisasa zilivyopangwa au uwape hiyo kazi Wataalamu wenyewe.
Leo nimekuwekea hizi picha 8 za Sebule tofautitofauti kutoka mataifa mbalimbali duniani kuona jinsi unavyoweza kujibadilisha pia kama haukua kwenye kiwango hiki.
Sebule ya pili ni hii hapa chini.. nimekubali sana ubunifu wa kutojaza rangi nyingi kuanzia kwenye carpet na ukutani, vitu vimekua simple kwa pamoja na imependeza sana.
Sebule hii ya tatu hapa chini ni kwa wale wenzangu tunaoanza maisha, kuishi kwenye nyumba ndogo au nyumba za kupanga zisizo na nafasi kubwa… kwa mchakarikaji yeyote wa mjini ukiweka kochi lako moja zuri, TV yako ukutani na nakshi za mbao unaweza kupata sebule ambayo sio rahisi kuichoka.
Usiache kuniambia umependa sebule namba ngapi mtu wa nguvu… niachie comment yako hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE