Ajali za mabasi ya mwendokasi Dar es salaam zimeendelea kumake headlines ambapo leo June 8 2106 mbunge wa viti maalum CCM Amina Mollel amelifikisha bungeni na kutusaidia kuipata idadi ya mabasi yaliyopata ajali na kiasi cha fedha zilizotumika kufanya matengenezo.
Amina amesema…>>>’Kwakuwa ajali nyingi zinasababishwa na madereva wazembe, mfano mzuri ukiwa ni Dar es salaam ambapo hadi sasa zaidi ya mabasi 30 yamepata ajali na gharama za matengenezo ikiwa ni zaidi ya milioni 90‘
‘Je, Serikali inatoa kauli gani kuwabana madereva wazembe wanaoisababishia hasara?‘
Majibu yametolewa na Waziri wa ofisi ya Rais tamisemi George Simbachawene amabpo amesema…>>’Babaraba zile ni kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi na si vinginevyo, mtumiaji yoyote anayetumia barabara zile anakuwa amevunja sheria na hivyo yeye ndio anakuwa amegonga mabasi‘
‘Hawaruhusiwi kutumia barabara za mabasi yaendayo kasi zinazotumika sasa Dar es salaam, niwaombe waheshimu sana barabara hizo‘
ULIIKOSA HII? WAZIRI MWAKYEMBE HAJAPENDEZWA NA KAULI ZA WAPINZANI NA KAAMUA KUYATOA YA MOYONI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE