Baada ya Koffi Olomide kukamatwa Jumanne July 26 2016 nyumbani kwake Kinshasa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi na baadaye ikawa imeripotiwa kuwa amehukumiwa kwenda jela miezi 18 na adhabu hiyo kutajwa kuwa haitakuwa na faini.
Taarifa zilizoripotiwa ni kwamba Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali, BBC imeripoti kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.
Pamoja na baadhi ya vyombo vya habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela , Promoter wake wa nchini Kenya Jules Nsana amekanusha madai hayo na kusema kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko kwenye uchunguzi na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi Olomide.
Promoter Jules amesema Olomide alimpigia simu akamtaka aombe msamaha kwa wakenya wote kwa niaba yake…..>>>’Koffi alinipigia mwenyewe baada tu ya kuachiwa na akaniomba niombe msamaha kwa wakenya kwa niaba yake, tumpe siku mbili, tatu atazungumza mwenyewe’
ULIKOSA HILI KUHUSU KIFO CHA PAPA WEMBA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI