Bado imekuwa ngumu kupatikana kwa ufumbuzi wa beki wa pembeni aliyejiunga na Yanga akitokea klabu ya Simba Hassan Kessy, kujua hatma yake ni nini kama atacheza msimu huu au la, Kessy bado anakizuizi na Simba kwa kudaiwa kusaini mkataba akiwa ndani ya mkataba na Simba.
Kwa kawaida mchezaji mkataba wake ukiwa chini ya miezi sita anaruhusiwa kuongea na klabu nyingine lakini sio kusaini mkataba huku akiwa na mkataba na klabu nyingine, hivyo Kessy haruhusiwi kucheza licha ya kuwa alikuwa kabakiza siku ndani ya klabu ya Simba, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe ameweka wazi.
“Wengi wanafikiria kuwa Hassan Kessy tumemzuia kuichezea Yanga, sisi hatujamzuia yeye amezuiwa kwa mujibu wa kanuni ndio maana hata CAF hawakumruhusu kucheza katika michuano ya Kombe la shirikisho, kanuni ina ruhusu mchezaji akiwa na mkataba chini ya miezi sita kuongea na klabu nyingine lakini sio kusaini”
CHANZO: Star TV
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0