Baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti taarifa kuwa chama cha wananchi CUF kimeandaa kikao cha baraza kuu la uongozi la Taifa kesho jumanne 24 september 24 2016 ofisi za Vuga Zanzibar.
Leo September 26 2016 akisoma taarifa kwa niaba ya naibu katibu mkuu wa CUF, Prof. Lipumba amesema taarifa hizo sio za kweli na hakuna kikao halali cha kamati ya utendaji ya taifa kilichokaa kuandaa kikao cha baraza kuu.
Taarifa hiyo ya Naibu katibu mkuu wa CUF Tanzania bara imesema kuwa hivi sasa katibu mkuu Maalimu Seif Sharif Hamad yuko nje ya nchi. Kufuatana na katiba ya CUF yeye ndiye mwenye mamlaka ya katibu mkuu kwa sababu naibu katibu mkuu wa CUF, Tanzania bara kikatiba ndiye msaidizi namba moja wa katibu mkuu kama navyoeleza katiba ya CUF ya 1992 toleo la 2014 kifungu cha 95 (3).
Taarifa hiyo ya naibu katibu mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya imeeleza kuwa…….
>>>’Mimi sijaitisha wala sina taarifa ya kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika Zanzibar, kwa taarifa nilizonazo hakuna wajumbe wa kamati ya utendaji kutoka Bara waliokua Zanzibar wakati wa kikao hicho. Nachukua nafasi kuwajulisha wajumbe wote wa baraza kuu kuwa hakuna kikao chochote cha baraza kuu kilichoandaliwa na kamati ya utendaji ya Taifa ambayo kikatiba mimi ndiye mwenyekiti wake wakati katibu mkuu hayupo’.
ULIKOSA ALIYOYAZUNGUMZA PROF. LIPUMBA BAADA YA KUINGIA MAKAO MAKUU CUF? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI