Ni Jumatatu poa sana mtu wangu, bila shaka ulikua na weekend nzuri pia, na kwa wale watu wangu kutoka Kenya najua ilikua poa zaidi baada ya kushuhudia bonge moja la show ya Mombasa Rocks iliyobeba mastaa wakubwa sana akiwemo Chris Brown kutoka Marekani, Wizkid wa Nigeria, Vanessa Mdee na Alikiba kutoka Tanzania.
Pamoja na perfomance nzuri waliyoifanya mastaa hao, kumalizika kwa concert hilo kumeibua story mpya nyingi. Moja kati ya stori zilizotrend kwenye mitandao mara tu baada ya Breezy kutua Moi International Airport, iliibuka story kuhusu star huyo wa hit single ya Grass aint greener kusukuma simu ya shabiki wa kike aliyetaka kujipiga selfie na Chris bila ridhaa yake.
Issue nyingine kubwa ikawa ni kwenye mkataba wa show kati ya Chris Brown na Waandaaji wa tamasha la Mombasa Rocks, mkataba ulioibua mjadala kwenye social networks kiasi kwamba issue ya simu ya shabiki ikasahaulika kabisa.
Mkataba wa show hii ulisainiwa na kampuni mbili ambazo moja wapo ni ya nchini Uingereza na nyingine ni Wale Wasee Limited ambao ni mapromota kutoka Kenya.
Sasa nakusogezea hii kuhusu vitu alivyovitaka Chris Brown mpaka anatua Mombasa.
1. Kwa mujibu wa mtandao wa KENYANS, Chris Brown amelipwa kiasi cha Shilingi Milioni 90 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni moja na milioni mia tisa (1,931,212,410.84) za Tanzania ili kufanya show hiyo kwenye eneo la Mombasa Golf club kwa muda wa dakika 90 tu.
Na kwa mujibu wa mkataba, mpaka kufikia September 30, Chris Brown alikuwa amelipwa kiasi cha Shilingi Milioni 55 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni moja na milioni mia moja themanini (1,180,185,362.18) zilizojumuisha zaidi ya Shilingi milioni mia nne ishirini za usafiri wake na management yake pamoja na zaidi ya Shilingi Milioni mia saba hamsini za malipo ya awali.
Halafu kiasi kinachobakia ambacho ni zaidi ya Shilingi Milioni mia saba hamsini na moja (751,027,048.66) kimelipwa baada tu ya Chris Brown kufika Mombasa, Siku ya Jumamosi asubuhi.
2. First class sound pamoja na taa za kutosha kwenye stage atakayofanyia kazi.
3. Huduma ya chakula chenye hadhi ya kistar.
4. Ulinzi mzito sawa na anaopewa kiongozi mgeni anapotembelea nchi nyingine.
5. Sehemu yenye viwanja vya kisasa ambayo yeye na team yake watakua wakipumzika.
6. Huduma nzuri kwenye Hotel aliyofikia yeye na team yake pamoja na chumba chenye hadhi ya Rais, kimoja chenye hadhi ya kati kwaajili ya Manager wake, na vingine kwaajili ya wapambe wake, na Hotel yenyewe iwe na hadhi ya Nyota Tano.
7. Hotel aliyofikia ilitakiwa kuwa jirani sana na eneo ambalo atafanya show.
8. Makubaliano mengine yotote ambayo yanahusisha Interviews za Radio na TV yalitakiwa kupewa kibali na meneja wa tour wa Chris Brown.
ULIMISS KUMUONA ALIKIBA KWENYE CONCERT LA MOMBASA? NIMEKUWEKEA HAPA