Reporter wa AyoTV na millardayo.com Kagera ameripoti kutoka Mahakama ya hakimu mkazi Bukoba akisema kesi ya waliofungua akaunti feki ya kusaidia waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi Kagera imeahirishwa leo.
Ni Kesi inayowakabili watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutumia madaraka yao vibaya na imeahirishwa mpaka November 14 2016 kwa sababu upelelezi bado unaendelea na wanaendelea kuwa nje kwa dhamana.
Watuhumiwa hao ambao walifungua akaunti ya benki kinyume na utaratibu kwa ajili ya kukusanya michango ya maafa kagera kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo September 10 mwaka huu, ni aliyekuwa katibu tawala mkoa wa kagera Amantius Msole, Mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba Kelvin Makonda, mhasibu wa mkoa Kagera Simbaufoo Swai pamoja na meneja wa benki ya CRDB tawi la Bukoba Carlo Sendwa.
Mawakili wa watuhumiwa wameiomba mahakama kuweka wepesi katika kesi hiyo ili iweze kuisha haraka, kama hukuona jinsi watu walivyoteseka baada ya tetemeko jingine lililotokea baada ya la kwanza na kuleta hofu mpaka watu wakaamua kulala nje.