Wakati suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu likizidi kuchukua sura mpya kila siku, leo November 3 2016 Chama cha ACT Wazalendo kimekutana na waandishi wa habari na kulizungumzia suala hilo ambapo kimepinga utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo wa elimu ya juu ambao wanasema ukiachwa bila kupingwa na kuwakosesha watoto wengi wa maskini washindwe kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa itikadi, mawasiliano na uenezi wa ACT Wazalendo Ado shaibu amesema…. ‘takwimu zilizotolewa na bodi ya mikopo wanafunzi takribani 65,000 wenye sifa ya kujiunga na elimu ya juu, ni 20,000 pekee kati yao ndio wamepata mkopo, hali hii ikiachwa, maelfu kwa maelfu ya watoto wa maskini watalazimika kurudi nyumbani kwa kukosa mikopo’
VIDEO: Shirikisho la vyuo vikuu lataja hujuma bodi ya mikopo