Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma mjini ni moja kati ya viongozi ambao wamekuwa mara nyingi wakitumia vyema mitandao ya kijamii katika kuhabarisha jamii kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo ya kiutendaji lakini ni muda mrefu sasa umepita hatujamuona Zitto Kabwe akiandika chochote kupitia account zake.
Millardayo.com imempata kwenye exclusive interview ili kuzungumzia sababu za ukimya wake
‘Ni uamuzi ambao niliamua kuufanya baada ya kutofurahishwa na muswada wa habari ambao sasa ni sheria ya habari ambayo naiona ni sheria ambayo inaenda kubana uhuru wa watu kutoa maoni yao, nilitaka wananchi waendeleze pale nilipoishia ingawa nitarudi tena kwenye social media‘ –Zitto Kabwe
‘Sheria hii itaweza kuwadhibiti wanahabari na tasnia kwa ujumla wake, kama ikitumika vibaya inaweza kupelekea idadi kubwa ya wanahabari kutofanya hiyo kazi tena kwakuwa watatakiwa kuandikishwa na serikali‘ –Zitto Kabwe
‘Mimi wito wangu kwa serikali ningewasihi katika uandikaji wa kanuni wahakikishe yale makosa ambayo yamo ndani ya sheria yanarekebishwa ili kuweza kupata sheria ambayo utekelezaji wake hautowabana sana wanahabari pamoja na wananchi wengine wanaofanya kuhabarishana‘ –Zitto Kabwe
Ni kweli sheria hii imempa hofu Zitto mwenyewe hadi asipost chochote?>>>’Sio mimitu bali mtanzania yeyote kwasababu sasa hivi kupitia mitandao ya kijamii mtu yeyote anaweza kuwa mwanahabari lakini baada ya sheria kupita itakuwa ni mtu aliyeandikishwa pekee ndio ataruhusiwa kufanya kazi ya habari kwahiyo mimi imenitia hofu kwakuwa huwa naandika makala‘ –Zitto Kabwe
‘Sheria inataja social media lakini sheria hiyohiyo haionyeshi ni kifungu gani kinahusiana na social media, nilisimama kwenye bunge kupinga vitu kama blogs na social medias zisiingie kwenye huo mtego lakini baadhi ya mazaziri wakasema ni lazima iendelee kuwepo‘ –Zitto Kabwe
Unaweza kuendelee kumsikiliza Zitto Kabwe hapa chini…..
ZITTO KABWE ALIPOSIMAMA BUNGENI KUPINGA MUSWADA WA HABARI