Kila siku asubuhi huwa nazisogeza Headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account zangu za Twitter, Facebook na Instagram kupitia jina la @millardayo.
Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Magazeti yote ya Tanzania leo Nov 23 2016 na habari zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho pic.twitter.com/oMKtHZvtLq
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
Wabunge ‘washindwa’ kumtoa Lema Kisongo
MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, jana alishindwa kutoka mahabusu baada ya Mahakama Kuu kanda ya Arusha, kukataa kufanya marejeo katika uamuzi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kumnyima dhamana.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Moshi alitoa uamuzi huo mbele ya kundi la wafuasi wa Lema waliofika kusikiliza shauri hilo mahakamani, wakiwemo wabunge kadhaa.
Wabunge hao wa Chadema waliohudhuria mahakamani hapo jana kwa mara ya kwanza ni Dk. Godwin Mollel (Siha), Julius Kalanga (Monduli) na Cecilia Paleso na Joyce Munkya ambao ni wa viti maalum kupitia chama hicho.
Aidha, uamuzi huo ulitolewa katika mahakama ya wazi kutokana na shinikizo la wafuasi wa Lema baada ya awali Jaji Moshi kutaka kufanya shughuli zake ‘chemba’.
Majira ya saa nne asubuhi, Jaji Moshi alihamishia kesi hiyo kwenye chumba kidogo cha mahakama, lakini pakatokea vurugu kutoka kwa wafuasi wa Lema ambao walitaka kuingia ndani ya chumba hicho kusikiliza kesi hiyo.
Kutokana na hali hiyo, Jaji Moshi aliamua kurudisha kesi hiyo kwenye chumba kikubwa cha wazi, ili wafuasi hao wapate kusikiliza kinachoendelea.
Akitoa uamuzi huo, Jaji Sekela alisema anakataa ombi la Lema lililowasilishwa na wakili wake, Peter Kibatala, kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi yake na kufanya marejeo.
“Kutokana na Mahakama hii kupokea ombi la Lema, mahakama hii iliitisha faili na kuita pande zote mbili ili kusikiliza, lakini upande wa serikali walipinga sisi kufanya hivyo kwa madai Lema alitakiwa kukata rufani badala ya kupeleka maombi,”
“Nakubaliana na hoja hii na nafuta uamuzi wangu wa kuita pande zote mbili ili kusikiliza ombi hili, na kuagiza upande wa Lema kukata rufani.” – Jaji Moshi.
Alisema Lema ana haki ya kukata rufani ili uamuzi wa kumnyima dhamana uliofanywa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambayo mwanzo ilikubali, lakini badala ya kutoa masharti ya dhamana walikatizwa na pingamizi la serikali.
Jaji Moshi alisema mshtakiwa anatakiwa kutumia haki yake ya msingi kukata rufani kama hakuridhika na uamuzi wa kumnyima dhamana.
Baada ya kumaliza kutoa uamuzi huo, kulitokea mkanganyiko kwa watu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo mahakamani, kwani badala ya askari kuita “kooorti” kwa sauti ili Jaji aondoke, alitoka kimyakimya.
Wakili Kibatala anayeongoza jopo la mawakili wa Lema, aliwaambia wanahabari na wafuasi wa Chadema baada ya uamuzi wa jana kuwa wanakata rufani kwa hati ya dharura na kuwasilisha jana hiyo hiyo, ili mteja wao apate haki yake.
GEREZA LA KISONGO
Lema aliondoshwa mahakamani saa 5:42 asubuhi, kwa ulinzi wa askari polisi wa kutuliza ghasia (FFU) na askari Magereza, huku wafuasi wake wakimpungia mkono, akipelekwa mahabusu katika Gereza Kuu la Kisongo.
Lema hakusita kuongea mbele ya askari hao, akiwataka wafuasi wake wasiogope, wajipe moyo, watashinda.
Mke wake Neema, hata hivyo, alishindwa kuishi kauli ya Lema baada ya kuonekana mwenye huzuni. Alitafuta mahali na kukaa chini kwa masikitiko, huku wafuasi hao wakimfariji.
Awali wakati kesi hiyo ya uchochezi ilipokuwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Hakimu Desdery Kamugisha, alikubali kutoa dhamana kwa Lema lakini kabla hajatoa masharti yake, Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Paul Kadushi, alisimama na kuwasilisha nia ya kukata rufani kupinga utekelezaji wa uamuzi huo.
Alisema wanapinga Lema kupewa dhamana kwa sababu amekuwa akirudia kutenda makosa yaleyale anapokuwa nje, uamuzi ambao ulisababisha Mbunge huyo kwenda mahabusu.
Mawakili wa Lema walipoitaka Mahakama Kuu ipitie uamuzi wa Hakimu Kamugisha, Kadushi aliwasilisha pingamizi akiitaka isisikilize maombi hayo.
Akiwasilisha hoja zake jana mbele ya Jaji Moshi, Wakili Kadushi, akisaidiana na Wakili Matenu Marandu, alisema anawasilisha hoja mbili za pingamizi la mahakama hiyo kuendelea kusikiliza ombi hilo.
Alisema kimsingi maombi hayo yaliowasilishwa katika mahakamani hiyo yanakinzana na Sheria ya Mahakama ya Mahakimu.
Wakili Kadushi alisema uamuzi unaopinga kufanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wa kukubali kutompa dhamana Lema ni uamuzi mdogo na haukuwa na sababu za kukatia maombi.
#NIPASHE 10% tu ya wafanyakazi wa shirika la ndege Tanzania ATCL watasalimika kupunguzwa kazi hivi karibuni baada ya kukidhi vigezo vya kazi pic.twitter.com/sZbvRHdQlc
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#MWANANCHI Mfanyabiashara Shigongo na CCM wamefikia makubaliano ya kumaliza tatizo hili ambalo lilimfanya Shigongo kulalamika mitandaoni pic.twitter.com/k67JWkWRXc
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#MWANANCHI Chadema imesema kuanzia January itatumia kadi mpya za uanachama za kieletroniki zitakazofanya wakusanye Tsh. Bilioni 13 kwa mwaka pic.twitter.com/yM0G3aas6h
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#JAMBOLEO Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Eng. Deusdedit Kakoko amesema hataki kusikia dawa za kulevya zimepita bandarini hapo pic.twitter.com/1HXLxECB7G
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#TANZANIADAIMA Wakala wa Majengo Tanzania TBA imepiga marufuku watumishi wake nchi nzima kutumia simu za mkononi wakiwa kazini kuanzia 2017 pic.twitter.com/J63quoloZl
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#MAJIRA Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji EWURA wametaka wauzaji wa mafuta ya mitambo kutojenga vituo bila kupata kibali kutoka kwao pic.twitter.com/JV6e7sjBnu
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#TANZANIADAIMA Kada wa CCM na mfanyabiashara Eric Shigongo amedai yuko hatarini kufilisiwa baada ya chama hicho kutomlipa mabilioni yake. pic.twitter.com/ETXBnlei1j
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#NIPASHE Mahakama Kuu leo itasikiliza maombi ya upande wa utetezi ktk kesi ya kuvua samaki Bahari ya Hindi kutaka fidia ya Tsh. Bilioni 2 pic.twitter.com/MkXTdNGqFR
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#NIPASHE Waziri Elimu Prof. Ndalichako amewataka walimu na bodi za shule kutekekeza adhabu ya uchapaji viboko shuleni ili kudhibiti maadili pic.twitter.com/Dnb83wSyKD
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
#MWANANCHI Star wa HipHop Tanzania MwanaFA amesema aliandika "Dume Suruali" baada ya malalamiko ya watanzania juu ya hali ngumu ya maisha pic.twitter.com/HuolRBZcm0
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
VIDEO: Alice Tupa amekuchambulia Magazeti yote ya leo, November 23, 2016. Tazama hapa chini