Jeshi la Polisi Dodoma linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za uhalifu wa kuvunja nyumba na kuiba mali za watu, kaimu kamishna wa jeshi la polisi kanda ya Dodoma Kimora Ernest amesema wahalifu wote wamekamatwa ndani ya siku mbili mfululizo huku likiwataka wananchi waliowahi kuibiwa mali zao kujitokeza kubaini kama zipo kati ya zilizokamatwa.
‘Jeshi la polisi Dodoma tunawashikilia watu tisa kwa tuhuma mbalimbali zikiwamo za wizi, katika msako wa siku mbili tuliweza kufanya msako huo ambapo wanawake ni watatu na wanaume sita‘ –Kimora Ernest
‘Mtandao wa wahalifu hao ni mkubwa ukilinganisha na mitandao mingine kutoka mikoa mbalimbali, zoezi la msako linaendelea ili kumaliza msako huu‘ –Kimora Ernest
‘Mbinu wanazotumia wahalifu hawa ni kuvunja nyumba hasa nyakati za usiku na mchana pale wanapobaini kuwa wenyeji hawapo katika nyumba zao. Nitoe wito kwa wananchi kujiepusha na tabia ya kununua vitu mitaani visivyokuwa na risiti pia tuwatake wale wote waliowahi kuibiwa katika kipindi kama hiki wajitokeze kubaini kama kati ya mali zilizokamatwa ni zakwao‘ –Kimora Ernest
Unaweza kuipata stori kamili kwenye hii video hapa chini…
Uliikosa hii ya DC Dodoma kuhusu Mwanafunzi aliyebakwa na Mwalimu