Kutoka Dar es salaam leo December 13 2016 taarifa zilizotolewa na mtandao wa Jamii Forums zinasema Mwanzilishi wa mtandao huo Maxence Melo, amekamatwa na Polisi kwa kukataa kutoa taarifa za siri za watumiaji wa mtandao huo.
Maxine amenyimwa dhamana na atakaa rumande mpaka kesho atakapofikishwa mahakamani ambapo bado Mwanzilishi huyu ameendelea kushikilia msimamo kuwa kufanya hivyo ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi.
Mtandao huo umeripoti kuwa Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo Mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.
VIDEO: Tazama Makomando wa Tanzania walivyoonyesha uwezo wa kazi yao mbele ya Rais Magufuli