Leo December 30, 2016 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam limetoa taarifa ya oparesheni mbalimbali zilizofanywa ili kuhakikisha kuwa tatizo la uhalifu na wahalifu wanadhibitiwa na kutokomezwa kabisa kwa kipindi cha mwezi Januari 2016 hadi Desemba 2016.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM, Kamishna Simon Sirro amesema oparesheni zilizofanyika kwa kutumia vikosi mbalimbali vya Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM likiwemo Kikosi Maalum cha Kupambana na ujambazi wa kutumia silaha, Kikosi cha Mbwa na Farasi, kikosi cha Kuzuia Wizi wa Magari, Kikosi cha Askari Kanzu, Kikosi cha Intelejensia, Kikosi Maalum cha Kuzuia Wizi wa Ng’ombe, kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya na Kikosi cha Kuzuia ghasia( FFU) zimeweza kuleta mafanikio mbalimbali kama ifuatavyo:-
- Idadi ya watuhumiwa 7625 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kupatikana na bhangi kilogramu 2843 na gramu 78
- Jumla ya watuhumiwa 269 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya Madawa ya kulevya ya aina mbalimbali kama ifuatavyo: Cocaine kilo 3 gramu 255 na Heroine kilo 1 gramu 654
- Pia pombe haramu ya Gongo jumla ya lita 8547, mitambo 34 na watuhumiwa 5627 walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
- Watuhumiwa 126 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya Madawa ya kulevya aina ya Mirungi kilo 75 na gramu 254
- Jumla ya Silaha 67 na risasi 1076 za aina mbalimbali zilikamatwa pamoja na watuhumiwa 52 na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha/UGAIDI.
- Jumla ya wahamiaji haramu 105 toka mataifa mbalimbali walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
HALI YA UHALIFU KWA KIPINDI CHA JAN-NOVEMBA 2016 UKILINGANISHA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2015
S/NO. | KOSA | MWAKA 2015 | MWAKA 2016 | ONGEZEKO | PUNGUZO | ASILIMIA |
1. | MAUAJI | 327 | 291 | – | 36 | 11% |
2. | KUBAKA | 972 | 1030 | 58 | – | 6% |
3. | KULAWITI | 310 | 383 | 73 | 23.5% | |
4. | WIZI WA WATOTO | 26 | 19 | – | 7 | 27% |
5. | KUTUPA WATOTO | 27 | 15 | – | 12 | 44% |
6. | UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA | 204 | 127 | – | 77 | 37.7% |
7. | UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU | 1181 | 874 | – | 307 | 26% |
8. | UVUNJAJI | 5677 | 5355 | – | 322 | 5.7% |
9. | WIZI WA MAGARI | 392 | 321 | – | 71 | 18.1% |
10. | WIZI WA PIKIPIKI | 2644 | 2191 | – | 453 | 17.1% |
11. | WIZI WA MIFUGO | 197 | 163 | – | 34 | 17.3% |
Sababu za kuongezeka au kupungua kwa matukio haya kumetokana na juhudi za Polisi Kanda Maalum kuzuia na kupambana na uhalifu kwa kufanya doria pamoja na misako mbalimbali iliyopelekea kukamatwa kwa wahalifu wa makosa mbalimbali kwa kushirikiana na raia wema kwa kutupatia taarifa za siri ili kugundua makosa ambayo yanakera jamii. Jumla ya wahalifu 13,626 walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
Kufahamu zaidi kuhusu matukio yaliyotokea tazama video hii hapa chini.
VIDEO: Wajue madereva waliotajwa na jeshi la polisi kuongoza kwa ulevi wakati wa sikukuu. Tazama hapa chini