Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Majira, yenye kichwa cha habari ‘JWTZ wajengewa chuo cha mafunzo ya kivita Bagamayo’
#MAJIRA Serikali imeanza ujenzi wa chuo cha kisasa cha mafunzo ya kijeshi cha Jeshi la Wananchi JWTZ kinachojengwa Bagamoyo mkoani Pwani pic.twitter.com/ALmpNUlt6F
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
Gazeti hilo limeripoti kuwa waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi ameweka jiwe la msingi ktk mradi wa chuo cha kisasa cha mafunzo ya jeshi la wanancnhi wa Tanzania ‘JWTZ’ kinachojengwa Mapinga, wilaya ya Bagamaoyo Mkoani Pwani.
Akizungumza katika eneo lamradi Dkt. Mwinyi amesema mradi huo unafadhiliwa na jeshi la mkombozi la watu wa China ambapo chuo hicho kitatoa mafunzo maalumu kwa vikundi mbalimbali vya kijeshi ili kukabiliana na ufgaidi nchini.
Unaweza kuzipita habari nyingine kubwa zilizoandikwa kwenye magazeti ya leo
#UHURU Waziri Mkuu Majaliwa amesema nchi haina baa la njaa, awataka wananchi kutosikiliza taarifa za upotoshwaji kutoka kwa wafanyabiashara pic.twitter.com/lFeqcTG3UL
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#MAJIRA Zaidi ya watoto 110 wameripotiwa kupewa mimba na kujifungua wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha robo ya mwaka 2016 pic.twitter.com/W9DB3GyyGe
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#NIPASHE Bingwa wa kula pilipili duniani, Li Yongzhi kutoka China alianza kutumia kama kiungo cha kunogesha chakula kama watumiaji wengi pic.twitter.com/u4omFrSC8k
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#MTANZANIA Vibarua waliokuwa wakifanya kazi TANESCO K'ndoni walalamika kuachishwa kazi bila kuelezewa hatma ya malipo yao pic.twitter.com/sOvJkQtAqJ
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#TANZANIADAIMA Mbowe, Lowassa, Sumaye kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA inayokutana jijini Mwanza leo kujadili hali ya kisiasa nchini pic.twitter.com/Ncx5YM1pMO
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#UHURU Utafiti wa Shirika la Kukabiliana na Umasikini OXFAM umebaini kuwa pengo kati ya watu masikini na matajiri linazidi kuongezeka pic.twitter.com/3xaUOJ91Us
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#MWANANCHI Serikali imeruhusu tani mil 1.5 za chakula zilizokuwa zimehifadhiwa zianze kuuzwa ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya vyakula pic.twitter.com/QFxjqSc1Wq
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#MWANANCHI Ripoti ya utafiti iliyotolewa na Benki ya dunia 2016 imeonyesha 37% ya walimu licha ya kuwapo shuleni, hawakufundisha pic.twitter.com/KcMkV52B0V
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#MWANANCHI Zaidi ya wakazi 16000 jamii ya wafugaji Arusha wamelazimika kubadilisha mifugo kwa chakula ili kukabiliana na upungufu wa chakula pic.twitter.com/yfiPS2siil
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
#MWANANCHI Serikali imesema haina mpango wa kuziteketeza pembe za ndovu zilizokamatwa kwani si suluhisho la kukabiliana na ujangili pic.twitter.com/QcIvZ3gVOc
— millardayo (@millardayo) January 17, 2017
AyoTVMAGAZETI: Kilichojificha migogoro ya vyama vya upinzani, Serikali sasa yaanza kusambaza chakula, Bonyeza play hapa chini