Kila asubuhi mimi Millard Ayo nazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo na millardayo.com.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo January 20 2017 ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Mtanzania, yenye kichwa cha habari ‘Mume aua mke kisa kachumbari’
#MTANZANIA Stella Ibrahim adaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na mume wake Daniel, sababu yatajwa kuwa kachumbari iliyochacha pic.twitter.com/Cnd80lgPeN
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
Gazeti hilo limeripoti kuwa mkazi wa Mtaa wa Mageuzi, Manispaa ya Shinyanga, Stella Ibrahim (39), anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na mume wake, Ibrahim Daniel kwa kile kilichoelezwa kuwa alipewa kachumbari iliyochacha.
Tukio hilo limetokea juzi usiku, baada ya Daniel kumshushia kipigo mkewe akidai kuwa alimpa kachumbari ambayo haikuhifadhiwa vizuri na mboga nyingine aliyodai haina kiwango.
Mashuhuda wa tukio hilo, walidai kuwa Daniel alifika nyumbani akiwa amelewa, kisha kuulizia kachumbari ambayo alikula jana, ndipo mtoto wake, Elizabeth Ibrahim (13) akamwonesha kachumbari ambayo inadaiwa tayari ilikuwa imechacha.
Walisema hakufurahia kuona kachumbari hiyo imeharibika, ndipo alipoanza kuuliza kwanini haikuhifadhiwa vizuri, akisimulia mkasa huo, mtoto wa marehemu, Daniel Ibrahim (12) alisema baba yeke alifika nyumbani saa moja usiku, alimkuta yeye akiwa na mdogo wake, Elizabeth aliyemuhoji kwanini kachumbari imeharibika, lakini hakupata jibu.
‘Baada ya kuingia ndani, baba alimuuliza Elizabeth kachumbari aliyoiacha (Januari 16, mwaka huu) iko wapi, akaoneshwa. Baada ya kuiangalia aliiona imechacha, alitoka nje na kuchukua fimbo ambayo huwa anaiweka juu ya nyumba na kutaka kuanza kumpiga, kabla ya kuanza kumpiga Elizabeth alikimbia.;-Mtoto wa marehemu
“Baada ya Elizabeth kukimbia, mama ambaye alikuwa kazini alifika nyumbani, akamkuta baba akifoka, akauliza kuna nini, baba akasema kwanini hakupika mboga yenye kiwango na kwanini ulipikwa ugali mwingine wakati kulikuwa na ugali uliobaki mchana’;- Mtoto wa marehemu
Alisema kutokana na maswali hayo, mama yake alimjibu kwa hasira kwanini hakuacha fedha nyumbani za kununulia mboga yenye kiwango anachotaka.
‘Baada ya baba anayedaiwa alikuwa amelewa kudai kachumbari yake, mama aliingilia kati, akajikuta anaambulia kipigo… vipimo vya daktari vinaonyesha alipigwa na kitu kizito kwenye utosi, kichwa kikavimba na damu kavujia ndani kwa wingi’;-Mwenyekiti wa mtaa
#NIPASHE Serikali imesisitiza kuwa wizara zote zinatakiwa kuwa zimehamia Dodoma kabla ya February 28 na hakuna mabadiliko yoyote pic.twitter.com/itmxrPorBF
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#NIPASHE Wakati matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yakipungua, hali imebadilika na sasa watu hufukua makaburi ya albino pic.twitter.com/AyOKWPTkYv
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#NIPASHE Serikali imezifunga maabara 117 za watu binafsi mkoani Geita baada ya kuthibitika kutokuwa na sifa pic.twitter.com/RegwyzYdU5
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#NIPASHE Kamati ya bunge imeiagiza TPA kuhakikisha bandari ya Tanga inajiendesha ili kuipatia serikali mapato badala ya kutegemea ruzuku pic.twitter.com/t7SknnmI0S
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#JamboLEO Lissu akana mahakamani kuchapisha taarifa za uchochezi, zenye kichwa cha habari 'machafuko yaja Z'bar' asema yeye si mchapishaji pic.twitter.com/AWyhNBEcWX
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#MTANZANIA Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA yasema kwasasa matukio ya ujangili yamepungua nchini tofauti na miaka iliyopita pic.twitter.com/R5kUVxx6vw
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#HabariLEO Serikari imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya sheria ya bodi ya mikopo ili kuwezesha wanafunzi wa diploma kupewa mikopo pic.twitter.com/4gMkmjtsHe
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#MTANZANIA 79% ya wahitimu elimu ya juu nchini hawana ujuzi wa kufanya kazi ktk soko la ajira la kimataifa, husoma kwa nadharia bila vitendo pic.twitter.com/dOYdrNhtb1
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#HabariLEO Zaidi ya mil 41 zilizotolewa na TASAF kwa ajili ya kunusuru kaya maskini Bunda zadaiwa kutafunwa na viongozi waliopewa kusimamia pic.twitter.com/6JxV3imTGp
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
#NIPASHE BAWACHA kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya sheria kuhusu uhalali wa Rais Magufuli kuteua wabunge wawili wanaume wiki hii pic.twitter.com/rlahQKLxRA
— millardayo (@millardayo) January 20, 2017
AyoTV MAGAZETI: Vilio Mgodi mkubwa nchini kufungwa,Wanaosoma diploma kupewa mikopo, Bonyeza play hapa chini