March 13 2016, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alifungua rasmi ujenzi wa jengo la upasuaji wa Wagonjwa mahututi na mapumziko katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam na wakati huo alikua mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Leo January 29 2017 GSM FOUNDATION ambao ndio wamejitolea kwa hali na mali kulijenga jengo hilo kwa pesa za kitanzania MILIONI 420, wamemkabidhi Paul Makonda likiwa limekamilika.
Baada ya kukabidhiwa Mkuu wa mkoa Makonda akasema ‘Nimekabidhiwa jengo hili likiwa limekamilika hata mwaka haujaisha na hili ndio kusudi la Rais wetu John Pombe Magufuli watu wafanye kazi, nawashukuru sana GSM Foundation kwa mradi huu ambao utasaidia kupunguza vifo vya Mama na Mtoto‘
‘Mkimuona mkuu wa mkoa yuko na Wafanyabiashara jua yuko kwa maslahi yenu, yani ukiona tu kuna tajiritajiri flani amekaa na mkuu wa mkoa jua tu hapo Mkuu wa mkoa anampigia mahesabu ya kumuweka kwenye 18 ili mambo ya mkoa wetu yaende’ – Paul Makonda
TAZAMA JENGO LENYEWE KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI NA KUMSIKILIZA ZAIDI PAUL MAKONDA