Mchana wa January 29 2017 imetokea ajali ya Treni kwenye eneo la Ruvu ndani ya mkoa wa Pwani Tanzania ambapo Treni yenyewe inaitwa EXPRESS na ilikua ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wameelekea kwenye eneo la tukio ambapo AyoTV na millardayo.com zimempata Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogosa usiku huu kwenye eneo la tukio na kueleza yafuatayo.
- Kwenye ajali iliyotokea kuna Mabehewa ambayo yametoka nje ya reli na kuanguka lakini bahati nzuri kichwa cha Treni hakikuanguka na ndio maana unaweza kuona abiria hawapo.
- Abiria walihamishiwa kwenye Mabehewa ambayo hayakuanguka na wakaondoka na Treni hiyohiyo kuelekea Dar es salaam na nadhani wamefika kwenye mida ya saa mbili usiku, hapa kwenye eneo la tukio kuna Mabehewa ambayo yalitoka nje ya reli tu.
- Hapa ni Kilometa 73 kutoka Dar es salaam na ni maeneo ya Ngeta Ruvu na ajali hii ilitokea kwenye saa kumi kasoro jioni, kuhusu chanzo cha ajali…. kawaida tunafanya uchunguzi na tutawapa taarifa utakapokamilika na tuna Wataalamu ndani ya kampuni ya TRL watafanya kazi yao kwenye uchunguzi.
- Njia ya Treni imeharibika sana hapa na kuna Treni nyingine ya abiria itasafiri kutoka Dar es salaam kwenda bara kwahiyo usiku huu tutachokifanya ndani ya saa 24 tunataka tuwe tumesharudisha hii njia ili abiria na Treni nyingine za mizigo ziweze kupita na tunategemea mpaka saa tisa alasiri siku ya Jumatatu January 30 2017 Treni zipite kama kawaida.
- Katika ajali hii tumepata Majeruhi watano na aliyeumia sana ni mmoja na alipelekwa Tumbi Hospitali iliyopo Kibaha Pwani, Mtazame Mkurugenzi akiongea kwenye hii video hapa chini
UMEPITWA? AyoTV imempata aliyewaokoa Wachimbaji 15 waliofukiwa Mgodini Geita toka juzi, kaeleza mbinu walizotumia kuwapata