Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017 ilichezwa usiku wa February 1 2017 katika uwanja wa Stade de Amitie, mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya AFCON 2017 ilikuwa inazikutanisha timu za taifa za Misri dhidi ya Burkinafaso.
Mchezo wa Misri dhidi ya Burkinafaso ulikuwa na ushindani mkubwa kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu kutabiri ni timu ipi itaingia fainali, mchezo huo dakika 90 zilimalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, Misri ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 66 kupitia kwa Mohamed Salah lakini Burkinafaso wakasawazisha dakika ya 73 kupitia kwa Aristide Bance.
Kutokana na mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 kwa dakika zote 120, ililazimika mikwaju ya penati kutumika kuamua mshindi, Misri katika mikwaju ya penati walikuwa mahiri na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa penati 4-3, golikipa wao Essam El Hadary mwenye miaka 44 ambaye ndio mchezaji mkongwe kuliko wote AFCON 2017 ndio alikuwa Man of the Match kwa kuokoa penati mbili.
https://youtu.be/sqFdNZ7L06U
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4