Taarifa hii imetolewa na Idara ya habari maelezo Dar es salaam Tanzania ambayo iko chini ya Wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo na imeandaliwa na Mwandishi wa Idara hiyo Immaculate Makilika.
Taarifa ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Machi 8 Mwaka huu katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali na yataanzia katika Shule ya msingi Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.
Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio msingi wa mabadiliko ya kiuchumi ikilenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.
Maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya Wanawake vitaonesha bidhaa zao.
ULIPITWA? Bonyeza play hapa chini kumtazama Ridhiwani Kikwete akiongea kuhusu simu aliyopigiwa na Baba yake Rais mstaafu Kikwete baada ya kuona picha yake aliyopiga na Edward Lowassa.