Mchezo wa soka ni miongoni mwa michezo inayopendwa zaidi duniani huku wachezaji wakivuna kipato kikubwa kutokana na uhodari wao kuhakikisha wanatumikia klabu zao vizuri.
Nahodha wa Ureno na nyota wa club ya Real Madrid Cristian Ronaldo ametajwa kuwa ndiye mwanamichezo anayeingiza kipato kikubwa kwa haraka zaidi duniani akimzidi mpinzani wake katika soka Lionel Messi wa FC Barcelona.
Katika utafiti uliotolewa na Expert Market UK Cristiano Ronaldo anahitaji saa 45 au jumla ya siku za kazi 5.68 kuvuna pound milioni moja huku Lionel Messi akihitaji siku 5.96 kuingiza kiasi hicho.
Expert Market UK inawataja pia katika list hiyo madereva wa Formula One Lewis Hamilton na Sebastian Vettel, nyota wa American football Eli Manning na boxer Floyd ‘Money’ Mayweather.
Wengine ni nyota wa baseball Ryan Howard na nyota wa Real Madrid Gareth Bale anayetimiza idadi ya wachezaji wa soka watatu kwenye Top 10.
Nimekusogezea hapa list ya wanamichezo 10 wanaoingiza fedha nyingi kwa muda mfupi
Nafasi | Jina | Mchezo | Muda/siku za kuingiza paundi 1 million |
1 | Cristiano Ronaldo | Football | 5.68 |
2 | Lionel Messi | Football | 5.96 |
3 | Joe Flacco | American football | 7.23 |
4 | Lewis Hamilton | Formula 1 | 7.57 |
5 | Sebastian Vettel | Formula 1 | 7.96 |
6 | Eli Manning | American football | 8.60 |
7 | Floyd Mayweather | Boxing | 9.93 |
8 | Ryan Howard | Baseball | 12.72 |
9 | Gareth Bale | Football | 12.77 |
10 | Lebron James | Basketball | 13.71 |
VIDEO: Ulikosa kuyaona magoli ya Yanga vs Zanaco FC? Bonyeza play chini hapa kuyatazama.