Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu ambapo kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari mchana wa April 25, 2017 millardayo.com inakupatia fursa ya kutazama habari 3 kubwa zilizosomwa saa 7 adhuhuri kupitia TV za Tanzania.
Star TV Habari: Madai ya kunyanyaswa na Polisi
Wakazi wa Nzega Ndogo wametoa malalamiko kwa Mbunge wa Jimbo hilo Hussein Bashe kuwa, baadhi ya Askari Polisi wanaotembea na pikipiki maarufu kama PT na kuwanyang’anya pikipiki zao usiku. Wananchi hao waanalalamika pia kuombwa rushwa na Askari hao jambo linalowafanya kushindwa kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi. Malalamiko hayo ni ya muda mrefu kwa bodaboda hao ambao wengi ni vijana waliojiajiri.
Chanel 10 Habari: Chama cha Wakala na Forodha kuandaa mkutano wa kimataifa nchini
Chama cha Forodha kwa kushirikiana na Wizara ya Uchukuzi, wameandaa mkutano wa kimataifa ambao utafanyika kwa siku nne kwa lengo la kujadili namna ya kutumia usafirishaji na ukuaji endelevu wa kiuchumi. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na Wajumbe zaidi ya 300 wa ndani na nje ya nchi.
Star TV Habari: Wanafunzi watakiwa kupimwa afya
Kaimu Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni, Mwalimu Shida Samweli amesema wanafunzi wafanyiwe vipimo vya afya mara kwa mara ili kuwawezesha kufanya vizuri kwenye masomo yao. Mwalim Shida ameyazungumza hayo katika semina ya Afya iliyoshirikisha wadau mbalimbali wa elimu, wanafunzi na wazazi ikiwa ni kilele cha wiki ya elimu ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni leo April 25, 2017