Imeelezwa kuwa unene uliopitiliza unasababisha vifo vya mapema zaidi ya vifo vinavyosababishwa na kuvuta sigara, kwa mujibu wa utafiti mpya.
Watafiti kutoka Cleveland Clinic na New York University School of Medicine waliainisha sababu za vifo nchini Marekani wakitumia takwimu za mwaka 2014 na kubaini kuwa unene kupita kiasi ulisababisha vifo kwa 47% zaidi ya tumbaku.
Wakilinganisha data na juhudi za afya ya jamii, watafiti hao walisema tumbaku ingeweza kuongoza list kama isingeweza kuwekewa ukomo wa matumizi ya sigara duniani na kusisitiza kampeni kama hiyo ifanywe pia kupunguza vifo vitokanavyo na unene uliopitiliza.
Dr Glen Taksler, Mtafiti wa masuala ya Dawa kutoka Cleveland Clinic na kiongozi wa watafiti hao alisema: “Matokeo haya yanaendelea kuainisha umuhimu wa kupunguza uzito, kujikinga na kisukari na kula kwa kuzingatia afya.”
Matokeo hayo pia yaliainisha umuhimu wa kuhudhuria vituo vya afya na kuzingatia vipaumbele vinavyotakiwa kwa ajili ya mwili. “Ukweli ni, wakati tunafahamu sababu za vifo vya wagonjwa, kwa mfano; saratani ya titi au mashambulizi ya moyo, hatufahamu sababu zinazochangia, kama vile matumizi ya tumbaku, unene kupita kiasi, pombe na historia za familia.” – Dr Taksler.
VIDEO: Makomando wakionyesha uwezo mbele ya JPM kwenye sherehe za Muungano. Bonyeza play kutazama…
VIDEO: Onesho la Mbwa na Farasi kwenye sherehe za Muungano Dodoma. Bonyeza play kutazama…