Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF leo June 2 2017 mbele ya waandishi wa habari ametangaza kuwashukuru wote waliyokuwa wanaisapoti Serengeti Boys na kuichangia licha ya kutolewa katika mashondano ya AFCON U-17 kwa kanuni ya head to head.
Malinzi ambaye ameona kigezo cha uwiano wa matokeo ndio kimetumika katika michuano ya AFCON U-17 atapendekeza katika kamati ya utendaji kanuni hiyo itumike kuanzia msimu ujao kabla ya kuanza kuitumia kanuni ya tofauti ya magoli ya kushinda na kufungwa.
“Serengeti Boys baada ya kutolewa kwa sheria ya uwiano wa matokeo (head to head) na Niger kutokana na kufungwa goli 1-0 tukawa na point nne na Niger kwa hiyo kigezo cha head to head kikatuondoa, kwa hiyo kuanzia msimu ujao kamati ya Utendaji kwa timu za Ligi Kuu kama timu zikimaliza zikilingana point basi tutaangalia uwiano wa matokeo maana tunajifunza kutoka kwa wenzetu”
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera