Chama cha ACT Wazalendo kilikutana na Waandishi wa Habari DSM na kuweka bayana msimamo na kutoa tamko lao dhidi ya tukio la kupigwa mabomu Walemavu lililotokea Juni 16, 2017 DSM.
Walemavu hao waliandamana kwa lengo la kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ili kumfikishia malalamiko yao dhidi ya Askari wa Usalama Barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katikati ya jiji.
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho Ado Shaibu amesema chama hicho kinalaani kwa nguvu zote kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kuwatawanya walemavu hao.
>>>”Chama cha ACT Wazalendo tunalaani kwa nguvu zote kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya machozi na virungu kuwapiga watu wenye ulemavu, kuwatawanya, kuwaburuza na kuwafanyia vitendo visivyo vya kiutu pale walipojikusanya tarehe 16 mwezi huu katika Barabara ya Sokoine, Posta.
“Sababu ya lengo lao la kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ili pamoja na mambo mengine waende kueleza kilio chao cha kukamatwa mara kwa mara na Askari wa Usalama Barabarani na kilio chao cha muda mrefu cha kutaka maeneo ya kuegesha baiskeli zao zinazowasaidia katika kutembea katika mji huu.
“Kwa hiyo Chama cha ACT Wazalendo kinapinga vikali sana. Vitendo hivi ni vya aibu na havipaswi kutokea katika nchi ambayo kwa muda mrefu sana imekumbatia misingi ya Utu, Undugu na Mshikamano. Ni vitendo ambavyo hatukuwahi kuvizoea katika nchi yetu.” – Ado Shaibu.
Kitu Waziri Mwigulu amewaambia Watanzania kuhusu JPM, makinikia!!!