Leo June 20, 2017 Rais Magufuli ameanza ziara ya kikazi ya sikuu tatu mkoani Pwani ambako atazindua viwanda vitano pamoja na mradi wa maji wa mto Ruvu. Akiwa kwenye siku ya kwanza eneo la Bwawani Rais JPM amezungumza na wananchi kutaja vitu 15 ambavyo serikali yake inavifanya na itafanya.
Nimekukusanyia hapa chini unaweza kuvisoma.
'Mkionana wachache wanalalamika mujue Magufuli anafanya kazi, mkiona wachache wanalia wanasema Magufuli anatumbua semeni tumbua'-@MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Sizungumzii wana CCM ninazungumzia Watanzania wote tatizo alilonalo mwana CCM analo wa ACT, wa CHADEMA au wa CUF' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Tanzania ni ya pili kwa vivutio vya kitalii duniani ikiongozwa na Brazil, lakini vivutio hivi haviwanufaishi Watanzania' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Tanzania tuna kila kitu lakini angalieni sehemu tulipo, kuna mahali tulikosea na lazima tuparekebishe' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Tumelipa madeni ya serikali ambayo ilikuwa inadaiwa na wafanyakazi, tunataka tufike mahali tusiwe tunadaiwa kabisa' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Nimeongea na Waziri Mkuu wa Ethiopia ameniambia atatuma wataalam watusaidie kujenga bwawa la kuzalisha umeme wa kutosha' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Mimi nachukia sana wezi awe mwizi wa ndani au wa nje mwizi ni mwizi tu na wataula wachuya awamu hii' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Kibiti nawaambia kwenye awamu hii hawatapita najua walikuwa wachache na moto wameshaanza kuuona narudia tena hawatapita' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Tunanunua ndege na kujenga reli ya kisasa kwa kuwa sisi Tanzania ni matajiri ni lazima tuishi kitajiri tajiri' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Tumenunua ndege sita mpya hadi sasa zipo mbili zinazofanya kazi, nyingine inakuja na nyingine tatu zitakuja mwakani' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Tunaochelewesha maendeleo ya Kibiti na Rufiji ni sisi wenyewe, hakuna mtu atakayekwenda kuwekeza sehemu watu wanauana' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Mimi nimeshaalikwa kwenye nchi zaidi ya 50 lakini siendi mimi humu humu kwanza tunyooshane najua nikitoka watu watalala' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Kama Halmashauri haiwezi kujenga barabara waseme wasipewe fedha ili zibaki serikali kuu tujenge wenyewe barabara zetu' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Nataka kila kiongozi kwa nafasi yake ajitafakari anasaidiaje wananchi masikini na ukiona hupati jibu jiondoe mwenyewe' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
'Niliamua kwa makusudi kabisa Wizara ya TAMISEMI iwe chini ya Rais kwa sababu nataka kuisimamia mwenyewe kama Waziri' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) June 20, 2017
VIDEO: Umepitwa na majibu ya Waziri Mwigulu kuhusu Askari waliowapiga walemavu Dar? Bonyeza play kutazama