Sean “Diddy” Combs anaunza mwaka mpya kwa ku-sign dili la kinywaji cha gharama kubwa aina ya DeLeón.
Diddy amejijengea heshima kwenye kazi kama hizi kwa kuipa mafanikio Vodka ya Ciroc kwenye soko tangu 2007 kutoka kuuza cases 50,000 kwa mwaka hadi cases milioni mbili kwa mwaka 2013.
Muungano huu wa kibiashara umegawana umiliki kati ya kampuni ya Diddy’s Combs Wine & Spirits itamiliki 50% na kampuni ya Diageo itamiliki 50% ya kinywaji cha DeLeón.
Baada ya kutangazwa kwa muungano huo Diddy alisema,“Celebration is a cornerstone of all my businesses, and this joint venture is a natural extension of that portfolio”.
“DeLeón is an outstanding brand that appeals to those who love exceptional tequila in a distinctive bottle. Together with Diageo, we will take DeLeón to new heights.”
DeLeón kwa bei ya rejareja imetajwa kuuzwa kuanzia bei ya $120 kwenda juu.
Hapo chini Diddy akiwa kwenye kazi yake na Vodka ya Ciroc