Ni kazi yangu kuhakikisha haupitwi na habari yoyote, imenifikia hii kutoka jeshi la polisi jimbo la Nevada nchini Marekani walioamua kutangaza uhaba mkubwa bangi hivyo kuchukua hatua za dharura kukabiliana na tatizo hilo.
Jeshi la polisi huko Nevada, Marekani limetangaza dharura baada ya kutokea uhaba wa bangi, mahitaji yamekuwa makubwa kuzidi upatikanaji wake pic.twitter.com/BQxguWqYtv
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Marekani ina majimbo takaribani 25 ambayo yameruhusu matumizi ya bangi tangu mwaka 2001 hali ilifanya mahitaji kuwa makubwa tangu kuhalalishwa kwa mmea huo kwa matumizi ya kujiburudisha kwa binadamu ambao wamedai kuna upungufu wa wauzaji wa kutosha.
Sheria iliwapa wauzaji wa pombe ruhusa ya kuuza bangi lakini wengi hawatimizi mahitaji ya leseni kuweza kuuza bidhaa hizo. Idara ya kodi katika jimbo hilo ilitangaza dharura inayomaanisha kuwa maafisa watachukua hatua kukabiliana na uhaba huo.
Mauzo ya karibu dola milioni 3 yalikadiriwa ndani ya siku nne za kwanza baada ya matumizi ya bangi kuhalalishwa nchini Marekani, jimbo la Nevada nalo lilipiga kura ya kuhalalisha matumi ya bangi kama kiburudisho tangu November 2016.
BBC
VIDEO: Ilikupita hii ya jamaa aliyekamatwa na Bangi Kagera jinsi alivyojitetea? Bonyeza play kutazama
VIDEO: Mfungwa Mtanzania gerezani China alivyompigia simu Millard Ayo. Bonyeza play hapa kujua alichokisema