Unaambiwa kwenye mji wa Berlin huko Ujerumani kwenye supermarket tano yamepatikana mabox yaliyojaa ndizi ambamo ndani yake kulikua na dawa za kulevya zilizofichwa ambazo ni kilo mia moja arobaini.
Ni kosa ambalo limefanywa na wauza dawa au wasafirishaji wa hizo dawa wenyewe manake mzigo ulianzia kusambaa kwenye duka la jamaa anaeuza matunda kwa jumla kwenye mji hamburg ikiaminika ni baada ya kuwasili kwa meli kutokea Colombia.
Wafanyakazi wa hizi supermarket ndio walitambua haya mabox ambayo ndani yake ndio kulikua na hizo kilo 140 za unga aina ya Cocaine saa kadhaa baada ya ndizi kuanza kuuzwa kwenye maduka yao.
Unaambiwa mzigo huu wa Cocaine ndio mzigo mkubwa kukamatwa kwenye mji huu mkuu wa Berlin kwenye kipindi cha miaka 15, ni mzigo wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 8 na laki mbili.
Polisi wanasema kwa Ujerumani, wauza dawa za kulevya wana kawaida ya kutumia sana njia ya posta kusafirisha dawa za kulevya kwenye sehemu tofauti kuliko njia nyingine ambazo zimekua zikitumika.
Miaka minne iliyopita wafanyakazi kwenye supermarket nyingine waligundua dawa za kulevya zinazokaribia kilo themanini zilizokua zimefichwa kwenye maboxi ya ndizi, mzigo ulioingizwa Ujerumani kutokea Ecuador.