Stori kubwa ambayo inamake headlines kwenye mitandao ni kuhusu Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ kuvifungia vituo vya mafuta ambavyo havifuati utaratibu wa kutoa risiti za kielektroniki kutoka kwenye mashinde zilizofungwa moja kwa moja kwenye pump ‘EFPP’.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema zoezi hilo ni endelevu na wataendelea kukagua na kuvifungia vituo vyote ambavyo havifuati sheria na taratibu katika kutoa risiti za kielektroniki mpaka pale wahusika watakapofanya hivyo.
Aidha, Kayombo amesema katika zoezi hilo DSM walifanikiwa kufungia vituo 28 katika Manispaa ya Kinondoni lakini vituo 25 kati ya hivyo vinaweza kufunguliwa baada ya kufata sheria.
Manispaa ya Ilala vituo 31 vya mafuta vilifungiwa ambapo vituo 20 kati ya hivyo vimeonesha ushirikiano na vinaweza kufunguliwa huku manispaa ya Temeke vituo 9 vimefunguliwa kati 12 ambavyo vilifunguliwa.
TRA walivyovifungia Vituo vya Mafuta Mwanza!!!!