Leo July 20, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kwa mara nyingine kesi ya kutakatisha fedha na kughushi inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi July 31, 2017 baada ya upelelezi kutokamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Hata hivyo,mshtakiwa Nyange ameshindwa kuhudhuria Mahakamani kutokana na kuwa na hali mbaya ya kiafya ambapo Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi July 31, 2017.
Good news kwa Simba SC kutoka SportPesa imetangazwa!!
Hatutomuona Abdi Banda Simba msimu ujao, anaondoka Tanzania!!!