Kuna siku nilikua napiga stori na baadhi ya watu wangu wa nguvu ambao wamefanikiwa kufika Nigeria na kujionea jinsi kiwanda cha muziki wa huko kilivyo na taratibu zake ambazo wanaona ni tofauti na za nchi kama Tanzania, mastaa wa muziki ni wengi na kazi za kibalozi kwenye makampuni makubwa kama ya simu ni sehemu ya wanakopata mamilioni kila siku.
Waliniambia kampuni moja ya mawasiliano ya simu za mkononi inaweza kuwa na mabalozi hata watano ambao wote ni wasanii wa muziki hivyo inatoa fursa tofauti na nchi nyingine ambako akishapewa hilo dili msanii mmoja ndio mpaka amalize muda wake na nchi nyingi hawawatumii/hawatambui umuhimu wa kuwatumia Mastaa.
Wanigeria pia wameweza kuvuka mipaka mpaka kwenye mauzo ya nyimbo zao, nakumbuka siku moja nikiwa South Africa nilikutanishwa na Mnigeria ambae anamiliki kampuni inayouza nyimbo za Wanigeria kwenye kampuni zinazotengeneza simu za mkononi kama vile Samsung, yani ukinunua simu mpya tu ukiingia kwenye videoz na songs unakuta nyimbo za Wasanii wa Naija.
Baada ya hayo maelezo machache hapo juu naomba kukufahamisha kwamba picha hiyo ya kwanza ni ya magari matatu yanayomilikiwa na mastaa wa Nigeria, magari haya yote matatu yamepigwa picha yakiwa yamepaki sehemu moja.
Producer aliemtoa D’Banj >> Don Jazzy anaiendesha hiyo Aston Martin, Wizkid anaiendesha hiyo Porsche wakati D’Prince anaisukuma hiyo Mercedes Benz.
Katika stori kadhaa ambazo nimewahi kuzipokea, Mastaa wa Nigeria, Congo DRC, South Africa na Uganda ndio naona utajiri wao unaridhisha Afrika.