Usemi kwamba ‘Elimu haina mwisho’ umedhihirika baada ya ajuza wa miaka 91 Kimlan Jinakul kuhitimu masomo yake ya Shahada katika Chuo cha Sukhothai Thammathirat, Thailand baada ya kuihangaikia kwa miaka 10.
Taarifa zinaeleza kuwa Kimlan Jinakul alikuwa anatamani kusoma na kufika elimu ya juu tangu akiwa mtoto lakini hakufanikiwa ambapo hata baada ya kuolewa na kuwa na familia aliamua kusomesha watoto wake kwanza hadi ngazi ya Chuo Kikuu na baada ya wao kuhitimu ndipo alipoamua naye kujiunga pia Chuo Kikuu.
Watoto wake wanne kati ya watano wana Shahada za Uzamili na mmoja amefanikiwa kupata PhD nchini Marekani.
Kimlan alikuwa na umri wa miaka 72 alipojiunga Chuo Kikuu lakini kufuatia kifo cha moja wa mabinti zake aliacha masomo kwa miaka kadha kabla ya kujiunga tena na Chuo akiwa na miaka 85 ili kuendelea na masomo.
Ulipitwa na hii? Msimamo wa CLOUDS baada ya Makonda & Ruge kukutana