Utafiti mpya uliofanya nchini Uingereza kwa kutumia waajiriwa zaidi ya 2000 unaonesha kuwa jinsi umri wa watu unavyoongezeka ndivyo wanavyoendelea kuchukia kazi wanazozifanya.
Hali hii ya kutofurahia kazi zao huanza katika umri wa miaka 35 na huzidi sana pindi wanapofika miaka 55 na zaidi ambapo wengi wao huhisi hawathaminiwi na wala mchango wao hauonekani na hivyo suala hilo huuwa kabisa morali ya kazi.
Wanasayansi wanashauri kuwa mtu anapofikia kipindi hiki na kujisikia hali hii ni vyema kuwekeza nguvu nyingi na muda wao katika miradi inayowafurahisha ili kuepuka kuchoshwa na kazi ambazo wamekua wakizifanya kwa miaka mingi.
Ulipitwa na hii? Vitu vitatu vilivyofanya Nay wa Mitego awaite waandishi wa habari