Ishu ya Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wasiojulikana mchana wa leo Dodoma, watu mbalimbali wamekuwa wakielezea kupokea kwa masikitisho tukio hilo.
Mbali ya Watanzania kuonesha kuguswa zaidi na tukio hilo lakini pia nchi jirani ya Kenya imeguswa ambapo Chama cha Wanasheria wa Kenya kimeipokea kwa masikitiko taarifa hiyo.
Chama hicho kupitia kwa Rais wake Isaac Okero kimemwandikia Barua Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Godwin Ngwilimi kuonesha masikitiko ya Wanasheria wa Kenya.
Sehemu ya barua hiyo ilisomeka>>>Nimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za jaribio la mauaji ya Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mheshimiwa Tundu Lissu Mbunge. Taarifa zilizofika Nairobi ni kwamba ameshambuliwa na watu wenye silaha nyumbani kwake Dodoma…”
ULIPITWA? Polisi na RC Dodoma waongelea Tundu Lissu kupigwa risasi