Jumamosi ya September 9 2017 historia mpya imeandikwa kwa club ya Azam FC kwa mara ya kwanza baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kukubali Azam FC ianze kucheza mechi zao za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga katika uwanja wao wa Azam Complex Mbande Chamazi.
Azam FC leo imecheza dhidi ya Simba katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 dhidi ya Simba katika uwanja wa Chamazi lakini game haikufanikiwa kupata mbabe na kulazimika kwa sare tasa ya 0-0, huo ulikuwa ni mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu kwa timu zote mbili.
Mchezo wa leo wa Azam FC dhidi ya Simba unakuwa ni mchezo wao wa 19 kukutana kwa timu hizo katika Ligi Kuu toka walipokutana October 4 2008 na Azam kuibuka na ushindi wa magoli 2-0, kwa ujumla Simba kaifunga Azam FC katika Ligi mara 8 na kupoteza mara 5 na sare wametoka mara sita.
Kwa matokeo hayo sasa Azam FC na Simba zote zinafungana kwa kuwa na point nne kila mmoja katika msimamo wa Ligi Kuu wakitofautiana magoli, Simba sasa atacheza game yake ya tatu dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Uhuru wakati Azam FC wao watacheza na Kagera Sugar katika uwanja wao wa Chamazi.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0