Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 iliendelea usiku wa September 25 2017 kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Emirates, Arsenal ndio walikuwa wenyeji wa West Bromwich Albion na kucheza mchezo wao wa sita wa Ligi Kuu England.
Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli ambayo yote mawili yamefungwa na Alexandre Lacazette dakika ya 20 na dakika ya 67 kwa mkwaju wa penati, huo ukiwa ushindi wao wa tatu wa Arsenal katika game sita za EPL.
Ushindi huo sasa unaifanya Arsenal kufikisha jumla ya point 10 katika michezo yao sita waliyocheza hadi sasa katika EPL msimu wa 2017/2018, wakiwa wamepoteza game mbili na sare game mmoja, Arsenal wamesogea hadi nafasi ya saba.
Toka September 2016 hadi sasa Arsenal imepoteza game moja tu nyumbani ya Ligi Kuu England na imefanikiwa kushinda mechi 17 kati ya 21 ilizocheza na sare ni mechi tatu, hata hivyo toka September 2016 wamefanikiwa kufunga magoli 45 na kuruhusu magoli 15.
MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC September 21 Mwanza (2-2)