Kufuatia changamoto ya maji inayowakabili wanachi katika Wilaya ya Muleba, Kagera ambapo huwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na kushindwa kutekeleza majukumu mengine ya maendeleo kwa wakati, sasa changamoto hiyo imeanza kutafutiwa ufumbuzi.
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini, ambaye pia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa kampuni ya TBL kwa kushirikiana na wananchi wilayani humo wameanza kutengeneza miundombinu ya mradi wa maji hali wanayoamini itapunguza na kumaliza changamoto ya maji katika eneo hilo.
Aidha, Waziri Mwijage amewaomba Wanamuleba wengine wanaoishi nje ya Wilaya hiyo kujitoa kwa kuchangia ili mradi huo uweze kufanikiwa na kuwaondolea wananchi tatizo hilo huku wananchi wa Kata ya Mhutwe wakisema tayari wameshajitoa na kukubali kuharibu mazao yao na kutoa baadhi ya maeneo yao bila fidia na kuongeza nguvu zao pale zitakapoitajika ili mradi ufikie lengo na kuondokana na changamoto hiyo.
RC Mwanza alivyotekeleza ahadi yake kwa mlemavu wa miguu
Raisi Magufuli kafanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri