Baada ya mvua za siku mbili Dar es salaam daraja la Malecela liliharibika na kusababisha usumbufu mkubwa kwa ambao wamezoea kulitumia ila leo tumetangaziwa kwamba ujenzi uliochukua saa zisizopungua 24 umekamilika.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo October 30 2017 ametangaza kukamilika kwa ujenzi wa Daraja hilo ambapo Wananchi na Magari yao wameruhusiwa kulitumia kama kawaida ila wazingatie kwamba halina kingo hivyo wapite taratibu.