Asubuhi ya leo November 9 2017 kampuni ya Udalali ya YONO imeifunga kwa nguvu Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es salaam baada ya kudaiwa kodi ya pango iliyotajwa kuwa ni BILIONI 5.7
Kampuni ya Umma ya Ubungo Plaza Limited inayomilikiwa kwa ubia na Kampuni kubwa tatu NSSF, PSPF na NIC ndio inayomiliki jengo hilo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Ubungo Plaza Haroon Mgube amesema Blue Pearl alikua akilipa kodi ya pango vizuri tu kuanzia mwaka 2006 mpaka 2014.
Blue Pearl Hotel ilikua na mkataba wa miaka 15 kukaa kwenye jengo hilo na mkataba huo ungeisha 2021 lakini kutokana na kushindwa kulipa kodi ya pango kwa miaka iliyofatia, ameondolewa leo kwa nguvu huku mali zake zikishikiliwa…. Tazama hii video hapa chini kwa taarifa kamili
VIDEO: “Watu wanalia machozi, Serikali inasema mambo ya kilimo” – Magdalena Sakaya , Mtazame zaidi kwenye hii video hapa chini
UNAZITAKA BREAKING NEWS FASTAFASTA? Jiunge na Reporter wako Millard Ayo kwa kubonyeza kifuatacho SUBSCRIBE >>> YOUTUBE , APP YA MILLARD AYO, FACEBOOK , INSTAGRAM